Skip to content
BechoBook
Cover of Kilio cha Mwanamke

Non fiction

Kilio cha Mwanamke

by Idrissa Haji Abdalla

₹165₹30045% off
Just like new In stock
ISBN
9789987084975
Publisher
Mkuki na Nyota Publishers Limited

About this book

Sauti dhaifu ya kilio cha mwanamke ilinifikia pale nilipokuwa nimesimama karibu na vichaka vikubwa vilivyoshonana mbele yangu. "Hivi ni sauti ya binadamu kweli au ni mlio wa mnyama fulani?" Nilijiuliza swali hilo ingawa sauti ile niliyoisikia ilifanana sana na kilio cha mwanamke ambaye yuko katika maumivu makali. Hali fulani ya woga ilianza kuniingia polepole. Baada ya kuanza kupatwa na woga niliamua kumfuata bibi yangu ambaye nilimwacha akiendelea kukata kuni nyuma ya vichaka vingine vilivyokuwa kushoto kwangu.

Baada ya kutembea kwa hatua zisizozidi kumi nilimwona bibi akinifuata. Hapo niliamua kusimamana kumsubiri ili nim-wulize juu ya ile sauti niliyoisikia. "Nimesikia sauti kama ya mtu ambaye alilia kwa muda mrefu na mwisho akapoteza nguvu". Bibi yangu alieleza hivyo kabla ya mimi kumweleza. "Hata mimi nilisikia ile sauti, tena inaelekea ni sauti ya mwanamke. Hivi unavyoniona ndio nimeamua kutofuata tena hizo kuni, maana nimeanza kuogopa."

Author
Idrissa Haji Abdalla
Publisher
Mkuki na Nyota Publishers Limited
Pages
186
Binding
Paperback

More from this category

Non fiction

See all